Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Kombe la Dunia 2018: Ubelgiji 3-2 Japan
Kombe la Dunia 2018: Ubelgiji 3-2 Japan
Moja kwa moja
Ubelgiji yapunguza adahabu! 2-1 kwa sasa!, Ubelgiji 1-2 Japan
Jan Vertonghen amefunga bao la kupunguza mzigo!
Yoshida ndio Shida kwa Lukaku!, 68' Ubelgiji 0-2 Japan
Ubelgiji wajiboresha, 66' Ubelgiji 0-2 Japan
Kocha Roberto Martínez amefanya mabadiliko:
Marouane Fellaini na Nacer Chadli wameingia, kuchukua nafasi za Yannick Carrasco na Dries Mertens.
Ukistaajabu ya Japan!, 64' Ubelgiji 0-2 Japan
Ubelgiji imeorodheshwa nambari 3 kwenye msimamo wa FIFA kwa mataifa, lakini hilo halijaizuia Japan kuwakung'uta!
Lukaaakkkkkkkkkkkuuuuuu, amekosa na hajaamini!, 62' Ubelgiji 0-2 Japan
Japan imevaa sare ya samawati, si nyekundu!, 60' Ubelgiji 0-2 Japan
Kuna wengi wasioamini tunayoyashuhudia Rostov Arena, lakini ndio hali ilivyo kwa sasa. Ubelgiji sio waliovaa sare ya samawati, ni Japan!
Hili Kombe ni moto sana!, 55' Ubelgiji 0-2 Japan
Ujerumani
Uhispania
Ureno
Argentina
Wote walipigiwa upatu kulitwaa, lakini sasa wanakula kwa macho.
Ubelgiji, wachezaji wenye thamani, nao wanakaribia langoni!
Fellaini ataifaa Ubelgiji?, 54' Ubelgiji 0-2 Japan
Marouane Fellaini ni mmoja wa wachezaji wa akiba Ubelgiji!
Mdharau biu........., 53' Ubelgiji 0-2 Japan
Ubelgiji inakaribia zaidi kutoka Kombe la Dunia kuliko kufika robo fainali.
Inuuuiiiiiiiiiiiiiiiiiiii awazima tena Ubelgiji!, Ubelgiji 0-2 Japan
Wachezaji wa Ubelgiji wanawasiliana vipi uwanjani?, 50' Ubelgiji 0-1 Japan
Wachezaji huwasiliana kwa lugha ya Kiingereza ili kurahisisha mawasiliano na kuzuia ubaguzi.
Kiholanzi na Kifaransa ni lugha pekee zisizotumika!
Wengi wao akiwemo Kevin De Bruyne wametoka eneo la Ubelgiji linalokaribiana na Uholanzi, waliosalia kama Eden Hazard huzungumza Kifaransa, na wengine Kijerumani.
Haijalishi ni lugha zipi watakazotumia dhidi ya Japan, lakini wanadaiwa bado moja!
Hazaaaaaaaaaard, hadi mwamba wa lango!, 49' Ubelgiji 0-1 Japan
Genkiiiiiii Haraguchi na goli kwa Japan!, Ubelgiji 0-1 Japan
Kipindi cha pili, 45' Ubelgiji 0-0 Japan
Wachezaji wamerudi na mechi imeanza!
Kipindi cha Kwanza: Ubelgiji 0-0 Japan!, Muda wa mapumziko: Ubelgiji 0-0 Japan
Courtois akwepa aibu!, 45' Ubelgiji 0-0 Japan
Baada ya Caballero kufanya mzaha dhidi ya Croatia, Courtois amekaribia kuwa kipa mwingine wa kuchekwa Kombe la Dunia.
Alikaribia kuruhusu mkwaju wa Nagatomo kubingirika hadi langoni!
Robo fainali mlima mrefu kwa Japan, 43' Ubelgiji 0-0 Japan
Tangu ilipoonja utamu wa Kombe la Dunia kwa kucheza mara ya kwanza 1998, Japan imetoka hatua ya makundi (1998, 2006, 2014)
na
Kufuzu kwa hatua ya mchujo (2002, 2010, 2018).
Hajawahi kunusa robo fainali za Kombe la Dunia!
Hazard hapotezi matumaini lakini hapati mwanya Japan, 41' Ubelgiji 0-0 Japan
Bluu "Samurai" wa Japan waponea!, 37' Ubelgiji 0-0 Japan
Mabeki wa pande za kushoto na kulia Maya Yoshida na Gen Shoji wamekwama eneo lao. Eden Hazard na Yannick Carrasco wanawashughulisha!