Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Samatta afunga na kusaidia klabu yake Genk kufuzu Europa League
Mchezaji wa kitamataifa kutoka Tanzania Mbwana Ally Samatta amepata nafasi ya kucheza hatua ya makundi ligi ndogo ya klabu Ulaya, Europa League.
Hii ni baada ya klabu yake ya KRC Genk ya Ubelgiji kupata ushindi wa jumla wa 4-2 mechi ya kufuzu hatua ya makundi dhidi ya wapinzani wao Lokomotiva Zagreb ya Croatia.
Genk walipata ushindi wa 2-0 mechi iliyochezwa Alhamisi jioni.
Klabu hizo mbili zilitoka sare 2-2 mechi ya mkondo wa kwanza.
Samatta alifungia klabu yake bao la kwanza dakika ya pili naye mwenzake Leon Bailey akafunga la pili muda mfupi baada ya mapumziko.
Samatta pia alioneshwa kadi ya manjano dakika ya 69.
Droo ya hatua ya makundi itafanywa mjini Monaco baadaye leo Ijumaa mwendo wa saa tisa saa za Afrika Mashariki.