Msako waendelea baada ya watu wawili kuuawa kwa kupigwa risasi katika Chuo Kikuu cha Brown
Msako unaendelea baada ya wanafunzi wawili kuuawa na watu wengine tisa kujeruhiwa katika ufyatuaji risasi mkubwa katika Chuo Kikuu cha Brown huko Providence, Rhode Island.
Mshambuliaji huyo alifyatua risasi darasani karibu saa 16:00 kwa saa za huko (21:00 GMT) siku ya Jumamosi, katika jengo ambalo mitihani ilikuwa ikifanyika.
Chuo kikuu, kimojawapo kikongwe na chenye hadhi kubwa zaidi nchini Marekani, kiliwekwa kizuizini huku polisi wakimtafuta mshambuliaji huyo, ambaye bado hajakamatwa.
Wanafunzi katika sehemu za chuo kikuu wanaendelea kuambiwa wajikinge mahali hapo hadi polisi watakapowasindikiza kutoka eneo hilo.
Maafisa kutoka Hospitali ya Rhode Island walisema wengi wa waliojeruhiwa wako katika hali "mahututi lakini imara".