Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Mambo makuu matano yanayoakisi uhuru na usalama Afrika
Waafrika wako tayari kutoa uhuru wao wa kutembea kokote watakakona kuzungumza kile wanachokifikiri na kuwa tayari kufuatiliwa maisha yao kama haya ndio yatawafanya wapate usalama zaidi, kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na kikundi Afrobarometer. Haya ni mambo matano muhimu ya matokeo ya uchunguzi huo:
1.Waafirika wengi wako radhi kuuza uhuru wao ilimradi wapate usalama
Afrobarometer inasema kuwa kuwaambia watu wachague usalama au usalama ni mkakati unaotumiwa na serikali kuwashawishi watu kukubali masharti juu ya usalama.
Na utafiti umethibitisha madai makubwa kuwa wakati watu zaidi na zaidi wakijiandaa kuuza uhuru wao kwenda kule wanakopenda kwenda kwa ajili ya usalama wa nchi.
Wengi miongoni mwa wale waliofanyiwa utafiti- 62% - wako radhi kukubali kuwekwa kwa marufuku ya kutotoka nje na vizuwizi vya barabarani ili wapate usalama.
Mtizamo huu unadhihirika zaidi katika nchi ya Madagascar. Takriban 83% ya watu waliofanyiwa utafiti walikubaliana na kauli inasema "Wakati inapokabiliwa na tisho la usalama wa umma, serikali inapaswa kuwa na uwezo wa kutangaza amri za kutotoka nje na kuweka vizuwizi maalumu kuzuwia watu kutembea".
Kinachowchochea kujibu hivi, utafiti unasema, huenda ni kwasababu nchi " bado inajaribu kutoka katika limbo la kisiasa na ukosefu wa usalama ".
2.Waafrika wachache wanahisi wana uhuru wa kusema kile wanachokifikiria
Karibu katika nchi zote zilizofanyiwa utafiti, idadi ya watu wanaohisi kuwa wana uhuru wa kuongea wanachokifikia impungua .
Karibu theluthi mbili (68%) ya wale waliofanyiwa utafiti walisema watu wanapaswa "mara kwa mara" au "kila mara " kuwa makini ni kile wanachokizungumzia kuhusu siasa
Nchi ambako kumekuwa na ongezeko kubwa la watu kuongea kwa umakini zaidi ni Mali ambayo watafiti wameelezea kuwa imekuwa katika mzozo wa kisiasa tangu yalippotokea mapinduzi ya mwaka 2012 na wapiganaji wa kiislamu kuchukua mamlaka ya maeneo ya kaskazini mwa nchi.
Utafiti pia uliichagua Zambia na Tanzania kama nchi mbili ambako idadi ya watu wanaosema wanaweza kuelezea kile wanachokifikiria imepungua kwa kiasi kikubwa. Nchi hizi mbili , utafiti unaelezea kuwa watu "wanaangaliwa kutokana na kuongezeka kwa utawala wa kiimla wa serikali zao za sasa".
3. Idadi kubwa ya Waafrika wako tayari kuruhusu mawasiliano yao ya kibinafsi yachunguzwe
Takriban 43% ya wale waliofanyiwa utafiti huu wako tayari kukubali setrikali ifuatilie maisha yao kwa ajili ya usalama
Mali ilikuwa mstari wa mbele
Takriban 75% ya wale waliofanyiwa utafiti nchini Mali walikubaliana na kauli kuwa serikali inapaswa kuwa na uwezo wa kufuatilia mawasiliano ya kibinafsi, kwa mfano kwenye simu za mkononi, kuhakikisha watu hawaandai mipango ya ghasia .
Utafiti unasema kwamba "watekelezaji wa ghasia za itikadi kali ... huenda hutumia utashi wa wengi na haki za binadamu ".
4. Waafrika wachache hujali haki ya kujiunga na makundi
Utafiti unabaini kupungua kwa kwa uungaji mkono wa "haki ya kujumuika kwa uhuru ".
Hii ni haki ya kuunda au kuwa sehemu ya chama cha wafanyakazi, chama cha kisiasa au ushirika mwingine au kikundi cha kujitolea.
Au, kwa njia nyingine, dhana inahitajika ili kuanza kikundi cha maandamano ya upinzani, kama kile ambacho hivi karibuni kilichowang'oa madarakani viongozi wa Sudan na Algeria.
takriban 61% ya watu waliofanyiwa utafiti huu walikubaliana na kauli kuwa "Tunapaswa kuwa na uwezo wa kujiunga na shirika lolote liwe la la serikali au la ".
Hiyo ni njia ya "kawaida " ya kukata uungaji wa mkono wa uhuru wa kuungana - kuanzia 66% muongo mmoja uliopita katika nchi 20
Lakini Zimbabwe ilishuhudia kupungua kwa ''kiwango kikubwa " cha uungaji mkono wa uhuru wa kuungana.
tangu mwaka alipoingia madarakani mwaka 2017, serikali ya rais Emmerson Mnangagwa imekuwa ikiwakamata waandamanaji , hususan katika miji muhimu , ambao wanapinga sera zake za kunusuru uchumi.
Hata hivyo watu wa Zimbabwe, na majirani zao Afrika Kusini , hawakuwa wanaunga mkono kuuzwa kwa uhuru wao kwa minajili ya kupata usalama kuliko wakazi wa nchi nyingine waliofanyiwa utafiti.
5. Uungaji mkono wa uhuru wa dini umegawanyika
Watu wamegawanyika kwa idadi sawa juu ya uhuru wa kauli za kidini, huku 49% wakiunga mkono uhuru kamili na 47% wakiwa tayari kuvumilia ukomo wa serikali juu ya kauli za dini.
Viwango vya chini vya uungaji mkono wa uhuru wa kauli za dini ulikuwa katika nchi za Tunisia na Mali.
Zaidi ya 70% ya watu waliofanyiwa utafiti katika nchi hizi mbili walikubaliana na kauli inayosema "serikali inapaswa kuwa na mamlaka ya kudhibiti kile kinachosemekana kuwa ni mahali pa kuabudu, hususan kama muhubiri au waumini wanatishia usalama wa umma ".
Utafiti ulibaini kuwa hawa walikuwa ni kutoka nchi zenye waislamu wengi ambazo zimekuwa zikishambuliwa na makundi yenye itikadi kali - mfano mwingine, labda wa watu wa kuchagua usalama zaidi ya uhuru.
Zaidi kuhusu utafiti huu
- Utafiti wa Afrobarometer survey ulifanyika kwa kuzingatia maoni ya umma katika nchi 34
- Takribani watu 45,823 walihojiwa kati ya Septemba 2016 na Septemba 2018
- Watafiti walianza kukusanya maoni katika nchi 20 kati ya nchi zilizofanyiwa utafiti miaka 10 iliyopita.