Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
China imefanikiwa kutua mwezini lakini hiyo sio mipango yake ya siku zijazo.
China iliwasili kuchelewa kuhusu swala la anga za juu.
Lakini miaka 15 baada ya kutuma wanaanga katika anga za juu, China imekuwa nchi ya kwanza kufanikiwa kupeleka roboti katika mwezi.
Na katika muongo mmoja ujao inapanga sio tu kujenga stesheni mpya ya angani lakini pia kuanzisha kambi mwezini na kumaliza safari yake katika sayari ya Mars.
Muhimu, Xi Jinping , kiongozi mwenye ushawishi mkubwa tangu mwenyekiti Mao, ameunga mkono ndoto hiyo ya angani na ikiwa na uwekezaji usiopungua mabilioni.
Vyombo vya habari nchini China , wakati huohuo vimetaja ndoto hiyo ya angani kuwa mojawapo ya hatua kubwa ya kurejesha hadhi yake.
Hivyobasi , je ni kwa nini rais Xi Jinping na China wanataka kuweka alama angani na inamaanisha nini kwa mataifa mengine duniani?
China inatuma Ujumbe
Kulingana na Profesa Keith Hayward, mwanachama wa muungano wa jamii ya wanaanga nchini Uingereza, China ina malengo kama yale ya Marekani, Urusi na mataifa mengine.
Kwanza ni, mahitaji ya jeshi ambapo bila mahitaji hayo wasingewekeza fedha zote hizo.
Pili, njia nzuri ya kujionyesha ". "unaweza kusema kuwa hii ndio njia ambapo China inaonyesha uwezo wake'' , alisema ," Profesa Hayward
Tatu, Kuna raslimali ambazo hazijatumika na ambazo zinaweza kuwatajarisha wale watakaozitumia.
Kutuwa kwa chombo Chang'e-4 mwezi Januari 2019 ni kitu kizuri kilichohitajika kufanyika kulingana na Profesa Hayward.
''Hatukuweza kupeleka mtu mwezini lakini tunakaribia kufanya hivyo''. Pia inatuma ishara kwa majirani . Ni njia ya kuonyesha uwezo mdogo kwa njia ngumu,
China yenyewe imekuwa wazi kuhusu thamani ya uchunguzi wa anga za juu kwa lengo la kujiimarisha duniani.
''Uchunguzi wa mwezini unaonyesha uwezo wa taifa linalohusika'', Profesa Ouyang Zhiyuan mmoja wa wanasaynsi wakuu aliambia gazeti rasmi la serikali nchini 2006.
Ni muhimu kupandisha hadhi ya kitaifa ya taifa na kuleta mshikamo miongoni mwa raia.
Je ni mashindano ya anga mpya?
Sio ufahari pekee unaoweza kuyaletea wasiwasi mataifa kama vile Marekani.
Makamu wa rais Mike Pence alizindua mipango ya kuwepo kwa jeshi la angani la Marekani mwezi Agosti 2018 akisema kuwa linahitajika kwa sababu wapinzani wao wakuu wamefanya anga kuwa eneo linalozozaniwa.
Wakati huo ilionekana kuwalenga Urusi na rafikiye China.
Hatahivyo , licha ya ya mafanikio makubwa ya China na mipango yake ya siku zijazo, Profesa Hayward hadhanii kwamba Marekani ina haja ya kuwa na wasiwasi.
"Marekani bado ina uwezo mkubwa na ni mwekezaji mkubwa sio tu kupitia Nasa lakini pia kupitia Pentagon'' , alisema. Sidhani kwamba China inaweza kufikia viwango vya matumizi ya Marekani.
Lakini je hii ni anga mpya? Hatahivyo yote haya yalijiri siku chache tu baada ya Chombo cha Nasa kutua karibu na ulimwengu uliojaa barafu yapata kilomita bilioni 6.5 .
Wakati huohuo India imetangaza kuwa itatuma kundi la watu watatu angani kwa mara ya kwanza 2022. Inaonekana kila mtu anataka kufika mwezini.
Je hatua za China zinaweza kuwatia wasiwasi wachezaji wengine kuimarisha mipango yao ya siku za baadaye?
''Sidhani'', anasema Profesa Hayward. ''Ni vigumu kujibu kwa haraka , hapa unaangazia mipango ya muda mrefu''.
Bernard Foing, mkurugenzi mtendaji wa shirika la angani la Ulaya European Space Agency's International Lunar Exploration Working Group, amesema kuwa maendeleo yoyote ni mazuri kwa ulimwengu mzima kwa jumla.
''China imeonyesha hatua kubwa na ari ya kutaka kushirikiana na mataifa mengine'', alisema.
Kuna taifa moja ambalo haliwezi kushirikiana nalo, hatahivyo.Marekani nayo ina sheria ambazo zinalizuia shirika la Nasa kushirikiana na China kibiashara bila idhini kutoka kwa bunge.
Pia imependekezwa kwamba kwa lengo la kutoonekana kwamba inashindana na Marekani na Urusi , China haijioni kwamba inashindana na mtu.
''China inapigania maslahi yake badala ya mipango yake ya kushindana na mtu mwengine yeyote'', John Logsdon , mwanzilishi wa taasisi ya angani katika chuo kikuu cha George Washington .
Kwa maoni yangu , China inajipangia yenyewe kile inachotaka kufanya na sio kwa ushindani na mataiafa mengine.