Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
TRA yawataka wafanyabiashara wanaotumia mitandao ya kijamii kujiandikisha na kulipa kodi Tanzania
Wafanyabiashara wanaofanya biashara kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii nchini Tanzania wametakiwa kufika katika ofisi za Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ili wajiandikishe waanze kulipa kodi kwa mujibu wa sheria kama wafanyabiashara wengine wote.
Hayo yamesemwa na Kamishna Mkuu wa TRA, Charles Kichere alipokuwa akizungumza kupitia kituo cha redio cha Clouds FM kuhusu mbinu mbalimbali wanazokusudia kuzitumia ili kuhakikisha kuwa wanaongeza idadi ya walipa kodi na kuongeza Pato la taifa hilo.
Lakini akifafaanua hilo, Richard Kayombo mkurugenzi wa elimu kwenye mamlaka ya mapato nchini Tanzania (TRA), akizunga ana BBC amesema wafanyabiasha ambao tayari wana maduka na wamejisajili lakini wanafanya matangazo kupitia mitandao ya kijamii hao hawana tatizo lolote na wataendelea na biasahara zao kwa sababu wamejisajili.
"Wanafanyabiashara wanaotangaza na kuuza kupitia mitandao ya kijamii, hawana duka hawana ofisi lakini wana bidhaa na wanafanya biashara kwa njia ya mtandao bila duka wala ofisi ndio tunazungumzia."
Amesema utaratibu wa kodi haufuati mtaji bali mauzo na kama mauzo hayafiki milioni nne mfanyabiashara hastahili kujisajili lakini bali yanapofika milioni nne.
"Mfanyabiashara ana wajibu wa kujitokeza kujisajili na kupewa namba na kulipa kodi na kufanya biashara yake kwa uhuru," ameongeza.
Hata hivyo wafanyabiashara wengi wameelezea hisia zoa na kulamikia hatua hiyo ya TRA.
"Nimesikitishwa sana nikijiongelea kama mimi mtaji wangu ni mdogo sana na ndio maana nimesema labda nikodishe sehemu nifanye biashara iwe rasmi na siku zinasonga na hivyo nimeona kukaa tu bila kufanya shughuli yoyote hakutanipa faida yoyote, kwa sasa sisi kama vijana ambao hatuna ajira tunatumia mtandao kujiajiri sisi wenyewe," anasema kijana moja anayeuza nguo za mitumba kupitia mitandao ya kijamii.
Anasema vocha wanazotumia kununua mitandao tayari wamezilipia kodi na hivyo hawastahili tena kilipia biashara yao mitandaoni.