Jitihada za kuzuia maambukizi ya virusi vya ukimwi kisiwani Zanzibar

Kwa ujumla takwimu zinaonyesha kwamba Zanzibar ina kiwango cha chini cha maambukizi ya virusi vya ukimwi. Hata hivyo, serikali imesema, licha ya kuwepo kwa maambukizi madogo, lakini nguvu kubwa hivi sasa inaelekezwa kwa makundi maalumu.

"Kama tunavyojua Zanzibar kuna makundi haya matatu ambayo kiwango cha maambukizi ni kikubwa. Kundi la akina mama na akina baba pia ambao wanafanya mapenzi ya njia ya kuzamili lakini pia vijana wanaotumia madawa ya kulevya kwa kutumia sindano, na pia wavulana wanaofanya mapenzi na wanaume wenzao. Kwa hivyo mkakati wetu ni kuhakisha ya kwamba tunapunguza," kwa mujibu wake Ali Mbaruk ni kutoka tume ya ukimwi Zanzibar.

Visiwa vya Zanzibar vina historia ya muda mrefu ya muingiliamo na watu wa mataifa mbali mbali. Hata hivyo, wenyeji wanasema mila na desturi za wazanzibari zimechangia kuzuia kusambaa kwa kasi kwa maambukizi ya virusi vya ukimwi.

"Sisi kama wazanzibar tunaamini kwamba suala la kuwa na mwnamke zaidi ya mmoja pia ni sehemu ya mitikio wa kusema kwamba tunazuia. Kwa hiyo pia mtu anayekuwa na mke zaid ya mmoja, tunaamini miongoni mwao hao anakuwa ni mwalimu mzuri. Tunajua kuwa wake wanne kama atawatendea haki, wala hana kabisa jicho la nje. tena wanaume waongeze kabisa. waongezea wa pilia na wa tatu waongeze," Anasema Salma ambaye ni mratibu wa Jumuia ya watu wanaoishi na virusi vya ukimwi Zanzibar, ZAPHA.

Hata hivyo , Zanzibar haijasalimika Kwa asilimia mia moja. changamoto zilizopo visiwani humu hazina tofauti na zile za maeneo mengine ya nchi.

"Kwa upande wa sasa hivi unyanyapaa bado upo unaanzia ngazi ya familia pia ngazi ya jamii, ,mashule watoto wanasoma, pia ukienda katika madrassa bado ule unyanyapaa upo, bado ile kunyooshewa vidole ipo," anasema Sudi Khamisi Sudi ni mwanachama wa jumuia ya watu wanaoishi na virusi vya ukimwi Zanzibar.

Zanzibar licha ya kuonekana kuwa salama na mara kadhaa kupigiwa mfano katika majukwaa a ya kisiasa, lakini bado jitihada zinahitajika kukabiliana na maambukizi mapya hasa kwa makundi maalumu.

Shamra shamra hizi zimejumuisha watu kutoka matabaka mbalimbali wakiwemo watoto, vijana na wazee.

Azma kuu ikiwa ni kukumbushana kuhusu kinga, madhara na jitihada zinazofanyika kupambana na janga hili.

Maadhimisho haya yameenda sambamba na kutolewa kwa huduma za upimaji wa virusi vya ukimwi pamoja na magonjwa mengine kama vile kifua kikuu.

Kumekuwa na jitihada mbalimbali za kuhamasisha watu kupima afya zao.

Kwa ujumla takwimu zinaonyesha kwamba Zanzibar ina kiwango cha chini cha maambukizi ya virusi vya ukimwi. Hata hivyo, serikali imesema, licha ya kuwepo kwa maambukizi madogo, lakini nguvu kubwa hivi sasa inaelekezwa kwa makundi maalumu.

Hata hivyo, wenyeji wanasema mila na desturi za wazanzibari zimechangia kuzuia kusambaa kwa kasi kwa maambukizi ya virusi vya ukimwi.

Hata hivyo , Zanzibar haijasalimika Kwa asilimia mia moja. Changamoto zilizopo visiwani humu hazina tofauti na zile za maeneo mengine ya nchi.

Zanzibar licha ya kuonekana kuwa salama na mara kadhaa kupigiwa mfano katika majukwaa a ya kisiasa, lkn bado jitihada zinahitajika kukabiliana na maambukizi mapya hasa kwa makundi maalumu.