Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Je unajua mtoto wa kiume hubaleghe umri unaolingana na mamake?
Umri wa vijana kubaleghe unalinganishwa na wakati mama zao walipo vunja ungo, utafiti unaonyesha.
Akina mama ambao walivunja ungo mapema kuliko wasichana wenzao wanaishiwa kuwa na watoto wa kiume ambao wana:
• wana nywele za kwapani miezi miwili na nusu mapema zaidi
• wanatokwa na chunusi na sauti kubadilika miezi miwili mapema zaidi.
Kwa upande mwingine mabinti zao, huota maziwa miezi sita mapema zaidi.
Utafiti katika jarida la Human Reproduction umekagua data kutoka kwa akina mama 16,000 na watoto wao nchini Denmark.
Taswira ambayo wataalamu Afrika mashariki wanakubaliana nayo.
Umri stahiki ni upi wa vijana kubaleghe?
Mmoja ya wahariri wa ripoti ya utafiti huo, Dr Nis Brix, wa chuo kikuu Aarhus nchini Denmark, anasema: "kila daktari anapokutana na mgonjwa ambaye amewahi au amechelewa kubaleghe, daktari huulizia historia ya familia kuhusu suala hilo.
Umri wa wavulana na wasichana kuanza kubaleghe umekuwa ukishuka duniani kwa mujibu wa wataalamu.
Unalingana kutoka mtu hadi mtu, hatahivyo, inasadikiwa kwa wastani vijana huvunja ungo katika umri wa:
- 10 - 14 kwa wasichana
- 12 - 16 kwa wavulana
Wataalamu wametaja kwamba hili linatokana na kuimarika kwa afya na lishe bora katika ulimwengu wa sasa - lakini utafiti umeonyesha pia uhusiano kati ya kunenepa kupita kiasi na vijana kuvunja ungo mapema.
Kuna fikra nyingi kulihusu hilo, mojawapo ikiwa ni kuongezeka kwa unene miongoni mwa watoto kunahusiana na kubaleghe mapema kwa vijana.
Utafiti mnamo 2015, umebaini kwamba vijana kubaleghe mapema au kuchelewa kunahusishwa pia na hatari ya kuugua:
- Kisukari
- Kunenepa kupita kiasi
- Kufunga uzazi mapema
- Magonjwa au matatizo ya moyo
Msichana huambiwa amevunja ungo mapema anapobaleghe kati ya miaka 8-11, na kuchelewa ni kati ya miaka 15 na 19. Kwa wavulana umri stahiki wa vijana kubaleghe ni kati ya miaka 9 na 14.