Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Kwa Picha: Melania Trump alivyozuru mbuga ya wanyama
Hii ni mara ya pili kwa wake hao wa viongozi kukutana, kwani mara ya kwanza walikutana Ikulu ya White House mjini Washington DC wakati wa ziara ya kiserikali ya Rais Kenyatta mwezi Agosti mwaka huu.
Ajenda ya ziara ya Bi. Trump inawiana na harakati za shirika la Beyond Zero la Bi Kenyatta ambazo hushughulikia maslahi ya akina mama wajawazito, watoto wachanga, vijana waliobalehe, miongoni mwa masuala mengine mengi ya afya.
Kabla ya kusafiri kuja nchini Kenya, Bi Melania Trump alianza ziara yake katika bara hili huko nchini Ghana mapema wiki hii kabla ya kwenda Malawi.
Bi. Trump na mwenyeji wake Mkewe Rais Kenyatta pia watatafuta jinsi watakavyoimarisha ufungamano kati ya mashirika yao ambayo yanashughulikia masuala ya afya ya kina mama na watoto wachanga.
Mke wa Rais wa Kenya,Margaret Kenyatta akiwa ziarani na mke wa rais wa Marekani Melania katika mbuga ya wanyama nchini Kenya
Mke wa Rais wa Marekani Melania Trump na mke wa Rais wa Kenya Margaret Kenyatta walitembelea kituo cha wakfu wa kuhifadhi wanyama pori cha David Sheldrick.
Ziara ya Bi Melania Trump nchini Kenya inafuatia mashauriano waliyofanya na Mkewe Rais Margaret Kenyatta katika Ikulu ya White House wakati Mama wa Taifa aliandamana na Rais Uhuru Kenyatta katika ziara ya mwezi Agosti mwaka huu huko mjini Washington DC.
Bi Trump atatamatisha ziara yake ya bara Afrika kwa kuzuru Misri.
Atazingatia zaidi huduma za afya kwa akina mama wajawazito na watoto wachanga, elimu na jukumu linalotekelezwa na Marekani Kenya kujitosheleza katika utoaji huduma.
Hii ni mara ya pili kwa wake hao wa viongozi kukutana, kwani mara ya kwanza walikutana Ikulu ya White House mjini Washington DC wakati wa ziara ya kiserikali ya Rais Kenyatta mwezi Agosti mwaka huu.