Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Mbwa: Mambo 10 muhimu kuhusu rafiki huyu mkubwa wa binadamu
John Bradshaw ni mwanasayansi ambaye anayechunguza uhusiano kati ya binadamu na wanyama. Amekuwa akichunguza chanzo cha mnyama bora zaidi anayefugwa
Haya ni mambo makuu kuhusu mbwa.
1. Mbwa hakutokana na mbwa wa porini
Mbwa walitokana na mbwa fulani wa porini ambao walitoweka kutoka porini maefu ya miaka iliyopita
Leo hii mbwa wa porini huko Marekani na Ulaya ni binamu wa mbali licha ya waoa kuwa na DNA inayokaribiana kwa asilamia 99.
2. Huwa wa ukubwa unaotofautiana kuliko wa wanyama wengine wanaonyonyesha
Kwa sababu ya binadamu kuingilia kati kuna tofauti kubwa kati ya mbwa kuliko mnyama mwingine yeyote anayenyonyesha wa msituni au anyefugwa.
3. Wana "pua la pili"
Hiki ni kiungo kinachofahamika kama vomeronasal kilicho kwenye nafasi kati ya pua la mbwa na sehemu ya juu ya mdomo
Wanasayansi bado hawafahamu kazi ya kiungo hiki ni ipi, lakini baada ya kuwachunguza wanyama wengine kama paka na hutumia kiungo hiki kunusa harua iliyoachwa na mbwa wengine.
4. Si kuwa mbwawamepoteza kabisauwezo wa kuona rangi
Mbwa huona kijani kibichi, manjanona samawati ka mavile sisi huona, lakini macho yao hayawezi kuona rangi nyekundu ambayo mara nyingi huonekana kama rangi ya kijivu.
5. Mbwa 'hutabasamu'
Mbwa hutabasamu lakini si kwa sababu ya kama zetu .
Kulingana na mwanasayansi Dr John Bradshaw, mbwa anaweza kutabasamu kumshawiki mmilike wake kumunyesha mapenzi.
Kwa hivyo mbwa hawana furaha kila mara wanapotabasamu.
6. Mbwa wanaweza kuwa na matumaini
Sawa na binadamu mbwa wanaweza nao kuwa na matumaini ya kupata kitu fulani.
Utafiti wa kisayansi iligunduliwa kuwa mbwa fulani huwa wanapenda kuchunguza kitu licha ya kutokuwa na uwezo wa kupata chakula. Hata hivyo mbwa wengine hawakuwa na motisha ya kufanya hivyo.
Inaweza kuonekana kuwa mbwa wengine huwa na matumaini wa kufanikiwa huku wengine huwa hawatarajii lolote.
7. Mbwa hawajutii
Wamiliki wengine wa mbwa hutambua kile wanafikiri kuwa ni kujutia kwa mbwa lakini sayansi imeonyesha kuwa hilo hutokana na tabia ya mwenye mbwa.
Kujutia ni hali ngumu - mbwa huwa na hofu kuwa huenda akaadhibiwa bila kujua amefanya nini.
8.Hufanya urafiki sana na binadamu.
Mara mwana mbwa anajufunza kuwa wanadamu ni marafiki, hisia zake humwambia kuwa ndio njia tu ya kuweza kuishi na hufanya urafiki wa karibu na binadamu.
Hii ndiyo sababu mbwa wengine hukumbwa na msongo wakati akiachwa peke yao na uhusi kuwa wametelekezwa.
9. Mbwa hufanya urafiki usio wa kawaida na binadamu...
Viumbe wengine wanaonyonyesha hupata hisia kama za mapenzi na furaha lakini sasa mbwa wanajulikana kwa kuwa na hisia maalum ambazo huja kulingana na tabia na binadamu.
Wamiliki wengine wa mbwa wanaamini kuwa mbwa wao huwapenda lakini wanasayansi wana ushahidi tabia ya binadamu ndiyo huchangia pia tabia ya mbwa.
10. Ikiwa mbwahakutani na binadamu anaweza kuwa mbwa wa mwitu
Ikiwa mbwa hawezi kukutana na binadamu hadi umri wa miezi mitatu, anaweza kugeuka na kuwa mbwa mwitu.
Mfano mkuu ni mbwa wa anayejulikana kama Australian Dingo, ambaye ni aina fulani wa mbwa wa kufugwa ambaye aligeuka na kuwa mbwa wa msituni miaka elfu nne iliyopita.