Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Arsène Wenger apewa makaribisho makubwa Liberia
Aliyekuwa meneja wa Asenal Arsène Wenger amwwasilia nchini Liberia kabla a kutuzwa siku ya Ijumaa ambapo atapewa tuzo la juu nchini humo.
Wenger alikuwa kocha wa kwanza wa Rais George Weah kwenye klabu ya Ulaya baada ya Wenger kumleta Monaco 1988.
Weah ndiye mwafrika wa kwanza kushinda tuzo la Fifa la mchezaji wa mwaka.
Alistaafu kutoka soka mwaka 2003 na kuingia siasa.
Watu nchini Liberia wamekuwa wakisambaza picha za Wenger akikaribishwa nchini humo.
Wenger atapewa tuzo la hadhi ya juu zadi nchini Liberia katika hatua ambayo imezua maoni tofauti nchini humo.
Baadhi wanasema kuwa tuzo hiyo haistahili kupewa mtu binafsi kwa kile amemfanyia rais pekee.
Lakini tuzo hiyo si tuzo kuhusu uhusiano wa Rais na Wenger bali inatambua kile Wenger amechangia kwa michezo barani Afrika na kuwapa waafrika wengi fursa kwa mujibu wa waziri wa habari.
Rais Weah amesema kuwa Wenger "alinitunza kama mtoto wake" wakati alijiunga na Monaco, akisema kuwa "kando na Mungu, anafikiri kuwa bila ya Wenger hakuna vile nigefanikiwa Ulaya".