Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Wanasayansi wagundua sayari 10 zenye dalili za uhai
Wataalam wa maswala ya angani wametangaza ugunduzi wa sayari nyengine kumi angani ambazo huenda zinaweza kusaidia uhai.
Wanasayansi wa shirika linaloshughulikia maswala ya angani NASA wanasema kuwa data mpya iliochunguzwa kutoka kwa darubini ya Kepler inaonyesha sayari kumi zenye miamba ambazo zipo hatua chache kutoka kwa mkusanyiko wa nyota.
Sayari hizo ambazo zinatoshana na dunia, zote zipo nje ya jua katika mkusanyiko huo wa nyota.
Darubini hiyo ya Kepler sasa imegundua jumla ya sayari 50 katika maeneo tofauti yenye uhai angani.