Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Biashara ya pembe za Faru halali Afrika Kusini
Mahakama ya katiba ya Afrika kusini imelipinga jaribio la serikali la kutaka kuweka marufu kwa biashara ya pembe za faru katika matumizi ya ndani.
Matokeo yake ni kwamba pembe hizo za faru zinaweza kuuzwa ndani ya nchi huku marufuku katika biashara hiyo kimataifa ikiwa bado inaendelea.
Watunzaji wa wanyama pori hao wamedai kuwa, kuruhusu biashara hiyo kuendelea kufanyika kihalali kutaweza kupunguza idadi ya faru wanaouwawa kutokana na kwamba pembe za faru zinaweza kukatwa na kuacha wanyama hao hai.
Hata hivyo wahifadhi wa wanyama pori hawakubaliani na hatua hiyo.