Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Wabunge wapya wa Somalia waapishwa
Wabunge wapya wa bunge la Somalia, kwa sasa wanaapishwa katika sherehe zinazofanyika katika mji mkuu - Mogadishu.
Hii ni hatua muhimu mno ya kuelekea kumchagua Rais mpya.
Lakini uchaguzi wa wabunge bado haujakamilika.
Wengine walinyimwa fursa ya kuwania uchaguzi huo kutokana na kashfa mbalimbali.
Umoja wa Mataifa, Umoja wa Afrika -AU na asasi nyingine za kisheria, zimesema kuwa uhalali wa uchaguzi huo ni tete.