Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Mashambulizi ya Urusi yawatimua IS kutoka Palmyra
Wapiganaji kutoka kundi la Islamic State wamelazimishwa kuondoka kati kati mwa mji wa Palmyra saa chache baada ya jaribio lao la kuuteka mji huo
Mashambulizi ya ndege za Urusi yaliwalazimu wanamgambo hao kurudi nyuma.
Islamic State walikuwa wamedhibiti mji wa kitamadudi wa Palmyra kutoka mwezi Mei mwaka 2015 hadi wapolitimuliwa mwezi Machi.
Sasa shirika la kuangalia haki za binadamu linasema kuwa mashambuli makubwa ya ndege za Urusi yaliwalazimu Islamic State kuondoka mjini humo
Mji wa Palmyra unaonekana kuwa muhimu kwa kundi la Islamic State kufuatia kukaribiana kwa na maneo yaliyo na mafuta.
Islamic State iliharibu sehemu za kitamaduni za mji huo na kumkata kichwa mkurugenzi wa maeneo hayo ya kale muda wa miezi 10 waliodhibiti Palmyra.
Vikosi vya waasi jana Jumamosi vilisema kuwa vilikuwa vimezuia vikosi vya serikali katika maeneo wanayoyadhibiti mjini Aleppo.
Kamanda mmoja wa waasi alieleza sababu ya vikosi vya serikali kupunguza kasi akisema kuwa wanajeshi wengine wamepelekwa mjini Palmyra.