Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Wanaume 'wahasiwa' kwa pamoja Nairobi
Shughuli ya kufunga mirija ya uzazi kupitia upasuaji kwa wanaume (vasectomy), imetangazwa moja kwa moja kutoka chumba cha upasuaji mjini Nairobi, Kenya kama njia ya kuhamasisha watu kuhusu njia hiyo ya kupanga uzazi
Takriban wanaume 150 walifanyiwa upasuaji huo uliodumu muda wa takriban dakika 20 kwa kila mmoja.
Madaktari walifanya shughugli hiyo nyuma ya jukwaa lililofunikwa katika ukumbi wa taifa wa sanaa mjini Nairobi.
Wanaume nchini Kenya ambao mara nyingi huwa wana hofu ya kufanyiwa zoezi hilo la kupanga uzazi mara nyingi kwa kuhofia unyanyapaa.
Wale wanaoendesha kampeni ya zoezi hilo wanasema kuwa ndiyo njia salama ya kupanga uzazi.
"Wanaume wengi hudhani kuwa zoezi hilo humnadili mwananamme kuwa mwanamke," Jack Zhang ambaye ni daktari kutoka Canada aliiambia BBC.
Baadhi ya wanaume wana hofu kuwa watu hufa kwa wingi barani Afrika kwa hivyo kuna haja ya kuzaa watoto wengi.
Mwandishi wa BBC mjini Nairobi, anasema kuwa baadhi ya wanaume walishiriki zoezi hilo baada ya kuchochewa na gharama ya kulea familia kubwa.
"Mbinu ambazo mke wangu alikuwa akitumia kupanga uzazi, zilikuwa na madhara kwake, kwa hivyo mimi niliamua kwenda kukatwa mirija ya ya uzazi," mwanamme moja aliiambia BBC.